23/07/2025
JINA LA STORY:
💔 RUAAN – Safari ya Moyo
MWANDISHI:
✍ Rommy Nation
📞 WhatsApp: +255 787 508 085
---
EPISODE YA KWANZA: "MWANZO USIO NA MWISHO"
Katika usiku wa mawingu, mvua ikidondoka taratibu juu ya dari ya chumba chake cha hosteli, kijana mmoja aitwaye Rayan alikuwa akitazama dari kwa macho yaliyopotea. Muziki wa taratibu ulikuwa ukicheza pembeni – wimbo wake alioupenda sana: “RUAAN”. Kila mstari wa wimbo huo ulikuwa k**a ukimshona kwa sindano za maumivu.
“Nilikupenda… sio kwa sababu ulivyonitazama, bali jinsi ulivyogusa nafsi yangu kwa ukimya wako…”
Rayan alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili, chuoni, akisoma sheria. Lakini akili na moyo wake siku zote havikuwa darasani, bali kwa binti mmoja aitwaye Aira, ambaye alimpoteza miezi miwili iliyopita baada ya ugomvi mkubwa usiokuwa na maana.
Siku hiyo, Aira alimtazama Rayan kwa macho yenye ukali na maumivu:
> “Sikupenda nikuchukie… lakini kila ukimya wako unaniua.”
Tangu siku hiyo, Aira alitoweka. Simu haipatikani, mitandao haipo, na kila mtu aliyeulizwa alimjibu Rayan kwa mabega.
Lakini leo usiku, akiwa peke yake, Rayan alisikiliza wimbo wa “RUAAN” k**a ilivyokuwa desturi yake kila usiku. Kila mara akiufumba macho, sura ya Aira huonekana. Kicheko chake. Maneno yake ya mwisho. Na ile sauti aliyosema:
> “Siku ukinipoteza, hutajua nilivyokuwa zawadi hadi nitakapokuwa kumbukumbu.”
Katika harakati za maumivu na hisia kali, Rayan alianza kuandika barua. Lakini hii haikuwa barua ya kawaida – ilikuwa barua ya mwisho.
Lakini kabla hajaiandika mwisho, alisikia mlango wake ukigongwa. Mvua ilizidi kunyesha. Saa ilikuwa saa saba usiku. Hakukuwa na mtu aliyekuwa akimtembelea saa k**a hiyo. Alijongea mlango kwa hofu na hamu. Alipofungua mlango...
“Aira?”
Lakini hakukuwa yeye. Alikuwa dada mmoja aliyekuwa ameloa mvua, akilia, na kuanguka miguuni pake akiwa ameshika bahasha yenye jina lake…
> “Nimekuja… kwa niaba ya Aira…”
---
Je, huyu dada ni nani? Na bahasha ina nini ndani? Aira yuko wapi? Je,