TAFCA Shirikisho

Directions Contact the business

TAFCA Shirikisho Ukurasa rasmi wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania - TAFCA

29/09/2026
Wachoraji wa katuni 'A-list' nchini Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja leo hii mara baada ya kumpumzisha katunisti m...
18/09/2026

Wachoraji wa katuni 'A-list' nchini Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja leo hii mara baada ya kumpumzisha katunisti mwenzao Hayati Hussein Kinyanguli Tunzo almaarufu King Kinya kwenye makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa. King Kinya (swipe picha ya 2) alifariki dunia jana alfajiri jijini Dar es Salaam. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, amen.

07/09/2026
Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) hatimaye kimepata uongozi mpya baada ya kukamilika kwa uchaguzi wao ...
03/08/2026

Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) hatimaye kimepata uongozi mpya baada ya kukamilika kwa uchaguzi wao mkuu.

Uchaguzi huo uliosimamiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) umefanyika makao makuu ya CHAWASAWATA yaliyopo Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Viongozi waliokabidhiwa dhamana ya kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo ni:

Sebastian Daniel Mbebe (Mwenyekiti)

Aloyce Ngwikwi Chenda (Makamu Mwenyekiti)

Jacob Lumumba Kunduma (Katibu Mkuu)

Elias Cyprian Nchingama (Katibu msaidizi)

Christopher Dastan Chaduo (Mweka hazina)

Daria Noel Chinago (Mweka Hazina Msaidizi)

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama ni:
- John Benjamin Litunu
- Pius Vicent Kulagwa
- Liston Marunda Unison
- Ali kondo Kabongo
- Heriet John Mlawila
- Hassan Mohamed Uwesu

Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) Bi Rukia Walele anawapongeza viongozi hao kwa kuchaguliwa kwao.

MAONESHO MAKUBWA YA SANAA ZA UFUNDI!TANCRAFT inapenda kukualika kwenye maonesho makubwa ya sanaa za ufundi yatakayofanyi...
03/08/2026

MAONESHO MAKUBWA YA SANAA ZA UFUNDI!
TANCRAFT inapenda kukualika kwenye maonesho makubwa ya sanaa za ufundi yatakayofanyika Kunduchi Mall, Dar es Salaam kuanzia tarehe 28/8 hadi 30/8/2026
Ada ya ushiriki ni Tsh. 100,000/= kwa siku zote tatu (3)
Ada ilipwe kwenye Lipa namba (Yas) ya TANCRAFT: 227268892.
Kila mshiriki atapata meza na kiti. Mshiriki atakuja na bidhaa zake tu.
Kwa washiriki tafadhali jiandikishe mapema kwenye namba +255 787 905 707
Usikose fursa hii adimu, nafasi ni chache!

Tanzania Handicraft

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (MICAS)
Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania

06/07/2026

Kodi lukuki zinavyowaumiza wasanii wachongaji wa Tanzania.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (MICAS)
Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿
Ikulu Tanzania
Baraza la Sanaa (BASATA)

03/07/2026

Sekta ya utalii na sanaa nchini inatarajiwa kupata msukumo mpya kupitia Tamasha la Sanaa na Kazi za Ufundi litakalofanyika mwezi Oktoba mwaka huu, likiwa na dhamira ya kuhamasisha uchumi wa ubunifu, kutangaza utamaduni wa Tanzania na kuwafungulia wasanii masoko ya ndani na kimataifa.

Tamasha hilo linaandaliwa na Tanzania International Tourism Festival (TITF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA), likiwakutanisha wachongaji, wachoraji, wabunifu wa mavazi, watengenezaji wa vito, wafinyanzi na wasanii wengine wa kazi za mikono kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Grand Melia Arusha, Mkurugenzi wa Tanzania International Tourism Festival, Ibrahim Jamal, amesema tamasha hilo limebeba maono ya kuiunganisha sekta ya sanaa na utalii ili kuongeza thamani ya kazi za ubunifu na kuwapa wasanii fursa za kibiashara.

Amesema mbali na maonesho ya sanaa, washiriki watapatiwa mafunzo kuhusu uongezaji thamani wa bidhaa, ulinzi wa haki za kazi za ubunifu, pamoja na mbinu za kufikia masoko ya ndani na nje ya Tanzania kupitia sekta ya utalii.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TAFCA Shirikisho posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TAFCA Shirikisho:

Shortcuts

Share